Wednesday, 7 September 2016

PESA ZAWATIA UCHIZI WAREMBO HAWA WABONGO,WAWA JAMVI LA WAGENI


NDANI ya tasnia ya burudani Bongo, kwa sasa imevamiwa na wingi wa wasanii, wauza sura na wanamitindo wapya ambao wamejipatia umaarufu ndani ya muda mfupi hasa kutokana na kukua kwa kasi kwa mitandao ya kijamii. Wakiitumia mitandao hiyo kujitangaza, wamekuwa hawalali kwani ‘njaa’ yao kubwa ni mkwanja, tofauti na wadada wa kipindi cha nyuma ambao walitaka sana umaarufu, huku pesa ikiwa ni chaguo namba mbili. Wafuatao ni baadhi ya wanadada
‘hot’  wanaokutana kupitia kazi mbalimbali za sanaa ambao pesa zinawatoa akili na wako tayari kufanya lolote lile ili kupiga mkwanja.  
 
 LULU DIVA GIGY MONEY Huyu ni muuza sura kwenye video za Kibongo, ameonekana kwenye video nyingi zikiwemo, Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego na Inde ya Dully Sykes. Tofauti na kuuza sura, msichana huyu ni msanii akiimba wimbo uitwao Supu aliomshirikisha Matonya. Pia mtangazaji. Kuhusu kusaka pesa, Giggy anasema kuwa yuko tayari kufanya lolote lile kwa sababu dunia ya sasa kila kitu ni pesa na kama mtu hana mkwanja na thamani hana. “Maisha yamepanda na kila kitu ni gharama. Aisee kwenye pesa, bora punda afe mzigo ufike, niko tayari kupiga dili yoyote ile ya halali ndiyo maana natumia kila kipaji alichonijalia Mungu ili kuhakikisha nakamata mkwanja,” alisema Giggy.
 
LULU DIVA Ukitaja mavideo ‘vixen’ wakali kwa sasa Bongo, jina la mwanadada huyu haliwezi kukosekana. Ndiye ‘Official video queen’ kwenye kichupa cha wimbo uitwao Naogopa wa Mirror aliomshirikisha Barakah The Prince. Mwanadada huyu pia ni muigizaji na ameonekana kwenye muvi iitwayo Nikabu ya Kitale. Katika kutengeneza mkwanja, mara kadhaa amenukuliwa akisema hawezi kuweka usistaa du, anasaka mkwanja kwa kila hali na haachi kujichanganya, maana akiwa hana mkwanja hujihisi nusu chizi! HAITHAM Huyu ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao kazi zao zimebahatika kupata ‘air time’ nzuri kwenye media yingi. “Unajua kwenye maisha ya sasa huwezi kuwa tegemezi kabisa. Mara mapedeshee au wazazi. Inafikia hatua kila kitu unatakiwa kufanya mwenyewe. Kwa upande wangu pesa ni kila kitu na sanaa sifanyi kwa kumfurahisha mtu,” anasema.
ERYCAH Si jina geni kwa wapenzi wengi wa burudani Bongo. Tofauti na kuonekana kwenye kichupa cha Wimbo wa Saka Hela wa Mbongo Fleva, Linex, mwanadada huyu amewahi kukwaa skendo ya kutoka kimapenzi na mshikaji huyo, kabla ya kukanusha. Erycah ana diploma ya Record Management aliyoipata chuoni Magogoni, anasema mbali ya elimu, ameamua kujiingiza katika kuuza sura kwenye video kama biashara zingine na malengo makubwa ni kudaka mkwanja. “Dunia ya sasa imebadilika, wanadada hatutakiwi kuchagua kazi.
 Kama sina pesa kiukweli wakati mwingine huwa nahisi hata kuumwa,” anasema Erycah.
AMBER LULU Jina la mwanadada huyu machachari ni maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram. Kabla ya kufahamika anajihusisha na ishu gani hapa mjini, umaarufu wake ulitokana na skendo za kupiga picha za nusu utupu alizokuwa anazitupia kwenye mitandao na baadaye akaanza mishe za uvideo queen. Kuhusu mkwanja, Amber Lulu anasema bila kuwa nao, hakuna kinachofanyika kwenye maisha ya mwanadamu wa leo.  “Mh! Pesa ndugu yangu hata hakuna maneno ya kuizungumzia yakaisha, so kama sina pesa kwa nini nisiwe nusu chizi!” alimaliza Amber

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM