Monday, 5 September 2016

Papa Francis amtangaza Mother Teresa mtakatifu

Mother Teresa, mtawa wa Kikatoliki aliyeyatumia maisha yake kusaidia maskini nchini India, ametangazwa mtakatifu kwenye misa iliyoongozwa na Papa Francis huko Vatican.
MOTHER-TERESA
Papa alimtangaza mtawa huyo mzaliwa wa Albania, mtakatifu mbele ya umati mkubwa wa waumini wa kanisa hilo waliokuwa wamekusanyika kwenye kanisa la St. Peter, Jumapili jijini Vatican.
Makofi makubwa yalisikika baada ya mchakato huo unaojulikana kama ‘canonization’ kumalizika akisema, “Blessed Teresa of Calcutta to be a saint.”
Wakatoliki wakiwemo watawa wa Missionaries of Charity iliyoanzishwa na Mother Teresa, walikuwa wamekusanyika kutoka duniani kote kuhudhuria kutangazwa kwake mtakatifu, ikiwa ni miaka 19 tangu kifo chake.
Picha kubwa ya Mother Teresa, ambaye kanisa hilo linaeleza aliwahi kufanya miujiza kwa uponyaji wa wagonjwa wawili ilikuwa imetundikwa kwenye kanisa hilo wakati wa halfa hiyo kubwa.
Miujiza ya mtawa huyo iliwahi kuhusishwa na Monica Besra, mwanamke aliyekuwa na miaka 30 kutoka Kolkata aliyesema kusali kwa kumuomba Mother Teresa kulimponya. Kamati ya Vatican ilisema October 2002 kuwa haikuweza kupata uthibitisho wa kisayansi kuhusu kupona kwa mwanamke huyo.
Pia mwanaume wa Brazil aliyekuwa na uvimbe kichwani alipona baada ya ndugu zake kumuomba Mother Teresa amponye kwa mujibu wa gazeti la Avvenire, lenye uhusiano na kanisa katoliki.
Akizaliwa kwa jina Agnes Gonxha Bojaxhiu mwaka 1910, Mother Teresa alianzisha Missionaries of Charity kwenye maeneo duni ya Kolkata mwaka 1950.
Kutokana na kazi yake kusaidia maskini, Mother Teresa alishinda tuzo ya Nobel Peace Prize mwaka 1979.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM