Friday, September 9, 2016

Operesheni Dadapoa, Kakapoa Dar es Salaam Yashika Kasi

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linafanya operesheni ya kuwakamata wamiliki wa nyumba za kulala wageni wanaofanya biashara kinyume cha sheria.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Kanda hiyo, Simon Sirro, ilisema wamebaini baadhi ya nyumba za kulala wageni zinatumika kuhifadhi magenge ya majambazi na wahalifu wengine.

Alisema nyumba hizo zimekuwa zikitumiwa na wanawake na wanaume wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu ‘dadapoa’ na ‘kakapoa’.

“Ni wajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, hoteli, migahawa, vilabu vya vileo, kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisema.

Katika hatua hiyo, Kamishna Sirro aliwatahadharisha wafanyabiashara wa nyumba hizo kufuata utaratibu wa kupokea wageni kwa kuandika majina yao kwenye vitabu, namba za vitambulisho vyao na sehemu wanapotoka na pale watakapomtilia shaka mteja yeyote watoe taarifa kituo chochote cha polisi.

Aidha wenyeviti wa Serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wametakiwa kuwajibika na kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki  kwa lengo la kuimarisha ulinzi ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo Kamanda huyo aliwataka wageni wanaotoka mikoani kupuuza taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa polisi wanawakamata  watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni mchana kwa kosa la uzembe na uzururaji.

“Taarifa hizo si za kweli na watu wanaotoka mikoani nawaomba waendelee na shughuli zao kama kawaida na wapuuzie taarifa hizo, “alisema Kamishna Sirro.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.