Friday, September 30, 2016

Nay wa Mitego Awachana Tena Wenzake

Rapa Nay wa Mitego ambaye kwa sasa anafanya vyema na ngoma yake ‘Saka hela’ amefunguka na kusema kuwa amegundua kwenye muziki wa bongo fleva saizi kuna wasanii wengi maboya akimaanisha washamba.
NAY23
Nay wa Mitego alisema hayo kupitia kipindi cha ‘Ngaz kwa Ngaz’ kinachorushwa na EATV na kudai mwanzo walikuwepo wasanii wawili maboya lakini saizi amegundua wapo wengi sana kwenye muziki wa Bongo Fleva.
“Mwanzo walikuwepo kama wawili hivi lakini saizi nimekuja kugundua wapo wengi sana ni maboya, inawezekana wapo wanaoniona mimi boya lakini uboya wangu mimi una faida, wapo wasanii wengi wanadhani mimi boya kama mimi navyowaona wao ni maboya” alisema Nay wa Mitego
Mbali na hilo Nay wa Mitego alisema kuwa licha ya watu kuona anaandamwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lakini yeye hawezi kuwalaumu BASATA kwani amegundua kuwa yeye ni moja kati ya wasanii wachache ambao wanatolewa sana macho na watu wengi ndiyo maana amekuwa akifungiwa sana ngoma zake.
“Mimi mwenyewe huwa najiuliza kwanini mimi kila siku lakini hata watu wengine wamekuwa wakijiuliza hilo hilo, wimbo wangu wa ‘Pale kati’ unafanana na nyimbo nyingine nyingi tu ambazo zinaendelea kufanya vizuri mpaka sasa na hatukuwahi kusikia zikifungiwa. Lakini nimekuja kugundua mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao wanafuatiliwa sana na kutolewa macho hivyo siwezi kuwalaumu BASATA”. Alisema Nay wa Mitego
eatv.tv
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.