Wednesday, September 14, 2016

Mtaalam: Tetemeko la ardhi halina uhusiano na kupatwa kwa jua

Mjiolojia mwandamizi wa wakala wa jiolijia Tanzania, Gabriel Mbogoni, amefafanua kuhusu sintofahamu iliyopo ambapo baadhi ya wananchi wanadhani kutokea kwa tetemeko la ardhi kumekuja kutokana na kupatwa kwa jua kulikotokea mapema mwezi huu.
photogrid_1473798422678
Amesema kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya kupatwa kwa jua na tetemeko la ardhi. Mbogoni amelazima kutoa ufafanuzi huo kutokana na kuwepo taarifa mbalimbali zilizoripotiwa katika vyombo vya habari zikisema kuwa tukio lililotokea September 1 mwaka huu la kupatwa kwa jua, na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni katika mikoa ya Mwanza na Kagera, vinahusiana.
“Kwa kweli hakuna uhusiano wowote wa kupatwa kwa jua na matetemeko la ardhi,” alisema. “Tetemeko la ardhi linasababishwa na process ambazo zinatokea katika kina kirefu cha ardhi, ambapo huo ni mgandamizo unaotokana na nguvu za asili kwenye miamba katika kina kirefu. Huo mgandamizo unafikia pointi kwamba ile miamba inashindwa kuhimili ile nguvu za mgandamizo, na kupelekea kukatika kwa miamba inayosababisha ardhi kutikisika na mwamba unapokatika na ardhi inapotikisika ndio inakuwa tetemeko la ardhi,” alifafanua Mbogoni.
“Hakuna uhusiano kati ya kupatwa kwa jua na tetemeko la ardhi na hakuna namna ya kujua na kuweza kubaini tetemeko la ardhi linaweza kutokea lini na wapi,” aliongeza.
Kupatwa kwa jua kulitokea Septemba mosi mwaka huu na kuonekana zaidi huko Mbarali na tetemeko la ardhi limetokea Septemba 10 katika mikoa ya Mwanza na Kagera.
BY: EMMY MWAIPOPO
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

Total Pageviews

BONYEZA HAPO CHINI

TAZAMA FRANCIS CHEKA TV

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.