Monday, September 5, 2016

MAUWAJI YA DADA WA BILIONEA MSUYA,MFANYABIASHARA WA ARUSHA APANDISHWA KIZIMBANI KWA MAUWAJI HAYOMarehemu Aneth Msuya . 
Idadi ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya ambaye alikuwa dada wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Erasto Msuya maarufu bilionea Msuya, imeongezeka na kufikia wawili baada ya mwingine kuunganishwa nayo.Awali, Agosti 23, mwaka huu mshtakiwa Miriam Mrita (41) ambaye ni mke wa bilionea huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake.Hata hivyo, juma moja baadaye, mfanyabiashara wa jijini Arusha, Revocatus Evarist (40), alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo na kuuunganishwa na Miriam kwenye kesi hiyo.
Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo.
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

Total Pageviews

BONYEZA HAPO CHINI

TAZAMA FRANCIS CHEKA TV

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.