Friday, 9 September 2016

Mama Wema Afunguka kuhusu Beef yake na Man Fongo

NI Mama Wema Sepetu ambae ameingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutofautiana na mkali wa nyimbo za singeli, Man Fongo.
Sasa hapa tumefanikiwa kuipata video ikionesha Mama Wema akieleza tofauti yake na msanii huyo na kusema..
Kwanza kama utakuwa umesoma SMS yangu niliyomtumia nilimwambia kwamba Amani nakuheshimu sana hasa baba yako ambae mpaka sasa namuheshimu ila matusi ambayo umeanza kunitukana huko ulipo nimeyapata sasa endelea’
Sasa mimi ndio wakumshtaki maana amenisema vibaya huko walipokuwa na watu wake ziarani nimeumia sana mimi kama mzazi, Manfongo bado  mtoto mdogo sana kwangu na mimi’-
‘Kwa upande wa Man Fongo alisema…‘Wamemtumia meseji mama yake na Wema kwamba ninaisema familia yake wakati mimi Manfongo muhuni na muhuni siku zote hatuna muda wa kumzungumzia mtu, riziki yangu naisaka tangu nipo kitaani sina muda wa kujibishana na watu sasa Mama Wema ananitumia meseji za matusi’
Unaweza ukabonyeza play kuitazama hii video Mama Wema Sepetu akieleza tofauti yake na Man Fongo

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM