Tuesday, 6 September 2016

Madawa ya Kulevya Yadaiwa Kummaliza KR Muller wa Wachuja Nafaka na TMK Family

46886854-b82e-43b7-b577-0d364384f4fc.jpg
Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anajitambulisha kama Rais wa Rader Enteternment rapper KR Muller alimuambia msanii mwenzake mkongwe Juma Nature amuache kwanza afanye mambo yake Kisa kamwambia aaangalie asivutishwe madawa

KR Muller alikua kwenye kundi moja na JUma nature pamoja na Dollo kundi la Wachuja nafaka kabla ya TMK na Wanaume Halisi.

Juma Nature alimushauri na kumwambia huko anakoenda anaenda kuvutishwa unga, Jamaa KR alimmind sana, akamwambia aachane na maisha yake.

kuhusiana na ushauri aliopewa na rafiki yake ambaye waliimba wote katika kundi la TMK Wanaume family Juma Nature kwamba aangalie asijekulishwa 'unga' huko Rader Enteternment ambayo inamilikiwa na msanii TID.

Maneno hayo yameonekana dhahiri kumkera KR ambapo hajui kwa nini anaibuka na maneno kama hayo japo kupata ushauri si jambo baya.

''Mimi aniache tuu niendelee na mambo yangu kwani namuheshimu sana na sjui kwa nini amesema mambo yote hayo'' Amesema KR.

Awali Sir Nature alisema kwamba KR asidanganyike kuitwa Rais huko aliko na akaingia kwenye mtego wa kula unga badala yake atambue kwamba ana familia na ni mtu mzima sasa hivi.

Juma Nature alisikika akisema kwenye Mahojiano Msanii huyo alifunguka hayo baada ya Nature kusema kitendo cha KR kujiunga na Radar Entertainment, huenda kitamharibu asipokuwa makini "KR hawezi akatoka kwa sababu huyo boss wake mwenyewe hajitambui, inanishagaza kuona msanii huyo mkubwa T I D hadi leo anaishi kwa baba na mama, sasa atawezaje kusimamia wasanii ambao wanamajukumu yani wana wake na watoto? akasema kitu hicho ndisho kitamkwamisha KR na kuona kama anapoteza muda"

Siku si nyingi, KR ameumbuka baada ya Picha zake kuanza kusambaa mitandaoni.

Nimeamini asiyesikia la Mkuu huvunjika guu.

Hongera sana Juma Nature, ama kweli wewe ni kaka Kiongozi. Ile style yake ya Mapanga Shaa Sshaa..kwisha kazi.
9c8c9c85-ad01-4276-9406-c33b06f109c7.jpg 65b760ad-3708-4c32-9964-0c5714f1b430.jpg 450a4532-4a77-48af-8921-cce83938664f.jpg 
KR Mnyama ndani ya 18 ya camera. Hakika kaumbuka. Sijui atamwambiaje tena Juma Nature.

Tujikumbushe enzi zao

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM