Monday, 12 September 2016

Kocha wa zamani wa Simba, James Aggrey Siang’a amefariki

Taarifa kutoka Kenya zinasema aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba, James Aggrey Siang’a amefariki Septemba 10, 2016 alfajiri mjini Bungoma baada ya kuugua kwa muda mrefu.
csbq-qtuiaa_thn
Siang’a alikuwa ni miongoni mwa makocha walioheshimika Afrika Mashariki hususani Tanzania alipoingoza Simba kufanya vema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kufika hatua ya timu Nane Bora.
Kutokana na kifo hicho, Rais wa TFF Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF), Nick Mwendwa akieleza kwamba ameshtushwa na kifo cha Siang’a.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM