Thursday, September 29, 2016

Jamani sijafa hata mafua siumwi – Muhogo Mchungu
http://1.bp.blogspot.com/-MGAUbafqQ7I/UlBjTioWJhI/AAAAAAAAAVA/1D9odm0rpf4/s1600/IMG_3726.JPG
Muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Abdallah Makumbila alimaarufu kama Muhogo Mchungu amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki na kusema kuwa yeye saizi hasumbuliwi hata na mafua.
Muhogo Mchungu alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Supamix cha East Africa Radio amesema kuwa kwa sasa anafanya utaratibu wa kwenda kumshtaki mtu ambaye amesambaza taarifa kwenye mitandao kuwa yeye amefariki dunia.
“Mimi ni mzima wa afya njema kabisa mimi si marehemu kama watu wanavyosema ndiyo maana saizi Zembwela unaongea na mimi, saizi nipo Bagamoyo mzima wa afya njema kabisaa na katika wiki mbili hizi sijasumbuliwa hata na mafua, hata mimi nimesikia hizo taarifa za kifo changu na nimetumiwa mpaka picha, sasa sijui huyo alizusha hayo mambo alikuwa na maana gani, maana amezua taharuki kwenye familia yangu na katika jamii hivyo saizi nataka kwenda TCRA ili tuweze kumjua nani amefanya hivyo ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria” alisema Muhogo Mchungu.
Mbali na hilo Muhogo Mchungu amesema kuwa mitandao ya kijamii ni kama kisu ukiitumia vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii na kuwataka watu wataumie vyema mitandao ya kijamii ili wasilete madhara kwa jamii.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.