Monday, September 19, 2016

HAWA NDIO WANAWAKE 3 WALIOSHITAKIWA KWA UGAIDI KENYAKesi dhidi ya wanawake watatu walioshukiwa kuhusika katika shambulio dhidi ya kituo kimoja cha polisi katika mji wa bandarini wa Mombasa nchini Kenya mwishoni mwa juma, ilishindwa kufanyika kutokana na matatizo ya mawasiliano.
Mmoja wa washukiwa hafahamu kabisa Kiingereza au Kiswahili. Shukri Ali, ambaye ni mlemavu wa kutosikia, hakujibu lolote hata baada ya mfasiri wa ishara aliyeletwa mahakamani kumsaidia kuelewa kesi dhidi yake. Mtafsiri wa lugha ya Kisomali pia alikuwa mahakamani ili kuwasaidia washukiwa wawili, Saida Ali na Naima Mohamed Ali, ambao hawana uwezo wa kufahamu Kiingereza.

Shukri Ali, Saida Ali na Naima Mohamed Ali mahakamani, Mombasa
Jaji Emmanuel Mutunga, aliamuru Shukri Ali, kupelekwa hadi katika wachunguzi maalum wa kimatibabu, katika hospitali ya kitaifa ya Coast General. Wanawake hao watatu, ambao bado wanazuiliwa pia watachunguzwa na madaktari. Wanashtakiwa kwa kosa la kuwapa hifadhi wanawake watatu wanaodaiwa kuunga mkono kundi la Islamic State, ambao waliuwawa pale walipojaribu kushambulia kituo cyha polisi cha Mombasa siku ya Jumapili iliyopita.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21, wakati ripoti ya kimatibabu itakapowasilishwa mahakamani.

BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.