Saturday, September 3, 2016

Fella kumuachia Temba jukumu la kuisimamia Yamoto Band na ‘Mkubwa na Wanae Foundation


Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanae Foundation pamoja na Yamoto Band, Mkubwa Fella amesema tayari ameshampata mtu sahihi ambaye atamwachia mikoba yake ya kusimamia wasanii pale atakapostaafu. Fella akiwa na Temba
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, Fella amesema amemuandaa msanii wa Kundi la TMK Family, Temba kuwa mrithi wake.
“Kusema kweli mtu ambaye nitamwachia kijiti ni Temba, tayari imeshamuandaa vya kutosha na bado naendelea, kwa hiyo Temba tayari anaelewa nini anatakiwa kufanya muda ukifika,” alisema Fella.
Kwa upande wa Temba amesema yupo tayari kupokea majukumu atayoachiwa na bossi wake huyo.
“Mimi nipo poa tu, tayari nimeshazungumza naye kuhusu ili swala na naamini kila kitu kitaenda sawa,” alisema Temba.
Pia Temba alisema hata kama akiwa kwenye jukumu la umeneja hataacha kufanya muziki kwa kuwa muziki ni sehemu ya maisha yake.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.