Friday, September 9, 2016

Diva adai hamjui Ruby ‘Simjui na sijawahi kumsikia’

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ ambaye haishi vimbwanga, Alhamisi hii amefunguka kwa kudai kuwa hamjui msanii, Ruby ambaye aliwai kufanya vizuri na wimbo ‘Na Yule’. ruby-na-diva
Aidha amedai pia hamjui video queen Giggy Money ambaye hivi karibuni ameonekana kwenye video ya ‘Inde’.
Akiongea katika kipindi cha Papaso cha TBC FM Alhamisi hii, Diva aliulizwa endapo akikutana na Ruby ambaye ameachana uongozi wake wa zamani atamshauri nini, ndipo mtangazaji huyo alipojibu kwamba hamjui msanii huyo.
“How is Ruby? Simjui na sijawai kumsikia,” alisema Diva.
Hata hivyo, Diva hakueleza nini kilitokea kati yake na msanii huyo ambaye aliibuliwa na Serengeti Super Diva 2014 na baadae kupewa msaada zaidi na THT pamoja na Clouds FM.
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Total Pageviews

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.