Monday, September 5, 2016

Daraja la vioo la Uchina kufungwa ili kupisha ukarabati

Daraja la vioo la ZhangjiajieDaraja la vioo lililojengwa juu nchini Uchina ililosifiwa kwa kuvunja rekodi lilipozinduliwa siku 13 tu zilizopita limefungwa. _90842196_hi033705932
maafisa wanasema serikali inapanga kufanya ukarabati wa dharura wa eneo hilo na hivyo kufunga daraja hilo Ijumaa, ambapo tarehe ya kufunguliwa tena itatangazwa.
Lakini Kituo cha televisheni cha Marekani CNN kimesema kuwa msemaji amewaambia kuwa daaja hilo linaloelea juu “limekuwa likitembelewa na wageni wengi kupita uwezo wake “.
Amesema kuwa hakuna ajali iliyowahi kutokea na daraja halikuwa na ufa wala mpasuko wowote.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 430, ambalo ujenzi wake uligarimu $3.4 milioni, linaunganisha mabonde mawili ya milima ya Zhangjiajie, katika jimbo la Hunan.
Daraja hilo Linaeloelea umbali wa mita 300 kutoka kwenye bonde linasemekana kuwavutia sana waandaaji wa filamu.
Lilipofunguliwa lilisemekana kuwa daraja refu zaidi kwa kimo na upana zaidi lililotengenezwa kwa vioo duniani.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.