Wednesday, 7 September 2016

Christian Bella: Rais Magufuli ananikubali mpaka basi!

Christian Bella ameungana na Mrisho Mpoto kwenye orodha ya wasanii waliopo kwenye playlist ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
bella
Akiongea kwenye kipindi cha Bongo Beatz cha Star TV, Bella alisema Rais Magufuli anamkubali hadi basi! Amesema kwake kukubalika na Rais wa nchi ni heshima kubwa na kumbukumbu atakayoitunza milele.
Bella amedai ni muhimu kwakuwa hajawahi kuwambia kitu kama hicho na rais yeyote tangu aanze kufanya muziki. “Ni kitu kikubwa sana kwangu na sikutegemea,” alisema.
“Sijawahi kuambiwa na na rais yeyote, rais wangu ni Magufuli nampenda sana,” alisema Bella.
Hivi karibuni Mrisho Mpoto naye alionesha furaha yake baada ya Dkt Magufuli kumwambia kuwa anaupenda wimbo wake ‘Sizonje.’

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM