Tuesday, 27 September 2016

BREAKING NEWZZ: BARAZA KUU LA CHAMA CHA CUF LAMFUKUZA UANACHAMA PROFESA LIPUMBA


Baraza Kuu la chama cha CUF limemtimua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuanzia leo.

Katika kikao chake kilichoongozwa na Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed Katani kimepitisha uamuzi huo leo baada ya kuungwa mkono na wajumbe wote 43 waliohudhuria kikao hicho.
Mashtaka dhidi ya Lipumba yaliandaliwa na Sekretarieti ya chama yakimtuhumu kufanya vurugu, kuharibu mali za chama na kudharau barua ya wito wa chama kwenda kujitetea.
Mwishoni mwa wiki Lipumba aliongoza mashabiki wake kuvunja geti na milango ya ofisi ya chama hicho, Buguruni Dar es Salaam baada ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu, hatua iliyoungwa mkono na Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi.

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limefikia uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 10 (1)(c).

"AANDIKA JULIUS SUNDAY MTATIRO

MAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI TAIFA LA CUF lililokutana leo Zanzibar:

1. Limemfukuza uanachama, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba baada ya kujiridhisha kuwa amekiuka katiba ya chama kwa kuvamia Ofisi Kuu ya chama, kuongoza makundi ya wahuni yaliyopiga walinzi wa chama, kuvunja ofisi za chama na kufanya uharibifu wa mali za chama siku ya tarehe 24 Septemba 2016. (Baraza limejiridhisha kuwa Kikao cha Kamati ya Utendaji kiliitishwa kwa kufuata masharti ya Katiba na hakikuvunja masharti yoyote ya kuitisha Baraza Kuu na limejiridhisha kuwa Prof. Lipumba alifikishiwa barua yenye tuhuma zake lakini kwa makusudi amekiuka kuitikia wito wa baraza na hivyo kujipotezea haki ya kusikilizwa).

2. Limeukataa ushauri na mwongozo wa Msajili wa Vyama vya siasa alioutoa kwa chama kwa sababu umekiuka matakwa ya Sheria ya Vyama Vya Siasa ya Tanzania, hauna mantiki na mashiko ya kisheria na unakiuka matakwa ya katiba ya CUF.

3. Limesisitiza kuwa Kamati ya Uongozi liliyoiunda ndiyo inayotambulika kikatiba hadi hapo atakapochaguliwa Mwenyekiti mpya wa CUF.

MY TAKE;
Chama cha siasa huendeshwa kwa vikao halali siyo maamuzi na matakwa ya mtu.

JS Mtatiro"

 

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM