Friday, 9 September 2016

Aunty Ezekiel Afunguka Sababu ya Yeye Kujiachia Enzi Zile

Nyota wa filamu nchini Aunty Ezekiel amefunguka kuwa kipindi cha nyuma kabla ya kuwa na mahusiano na Mose Iyobo na kabla ya kupata mtoto alikuwa akijiachia sana kwa lengo la kutafuta kiki na wala hakuwa na woga wa kufa kwani hakuwa anategemewa na mtu.

Aunty Ezekiel alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz na kudai kuwa alikuwa akivaa vibaya na kuwa na skendo mbalimbali kwa lengo la kutafuta kiki na kufahamika zaidi lakini saizi yeye hafanyi tena mambo hayo kwani amekuwa akiogopa kifo kwa kuwa anatambua nyuma ana mtoto ambaye anamtegemea na anategemea malezi yake, ndiyo maana ameamua kuachana na mambo hayo.

“Kwa sasa nimeacha kiki za ajabu ajabu saizi naangalia maisha ya familia, saizi nimekuwa mama naangalia vitu kwa upande mwingine kesho na kesho kutwa mwanangu amekua, amekuta hayo matukio, ohh mama yako alivaa kichupi, mama yako alikuwa hivi alikuwa vile ataiga nini mtoto kutoka kwangu? Kwa hiyo saizi naangalia mara mbili ya pale nilipokuwa mwanzo. Hata zamani nilikuwa ni mtu ambaye nasema aah si tunaishi mara moja tu hivyo kesho na kesho kutwa nikifa nasema potelea mbali lakini saizi nakiogopa kifo kutokana na kwamba nina mtu nyuma yangu ananitegemea” alisema Aunty Ezekiel

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM