Friday, 30 September 2016

Alichofanya Mfakanyazi wa Shirika la Ndege la Ethiopia Alipookota Bahasha Yenye Milioni 21.8


Shirika le Ndege la Kimataifa la nchini Ethiopia limempongeza hadharani mmoja wa wafanyakazi wake kwa kurejesha fedha kiasi cha dola elfu 10 (sawa ni shilingi milioni 21.8) zilizokuwa zimesahauliwa na mmoja wa abiria aliyekuwa kwenye ndege.

Shirika la ndege la Ethiopia lilichapisha pongezi hizo kwenye ukurasa wake wa Facebook na kumpongeza mfanyakazi wa ndege hiyo Roza Shiferaw kwa kurudisha dola elfu 10 zilizokuwa ndani ya bahasha mali ya mmoja wa abiria.

Shirika hilo liliongezea kuwa kitendo alichokifanya Roza ni ushahidi tosha kuwa shirika hilo lina wafanyakazi wenye maadili na heshima kwa wateja wao.

Uongozi wa shirika hilo haukueleza zaidi kuwa abiria aliyesahau fedha hizo ni nani na mfanyakazi huyo alizikuta wapi.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM