Thursday, 25 August 2016

Shilole azungumzia bifu la Bill Nas na TID

Baada ya TID kudai kuwa Bill Nas hana shukrani, Shilole ameibuka na kumtetea rapper huyo wa label mpya,  ‘LFLG’.

Bado Bill Nas amekuwa akisema kuwa aliondoka Rada bila tatizo.

Akiongea na Perfecto TV, Shilole amesema Bill ni kijana mtulivu.

“Wanamuonea sana Bill Nas, kwasababu  ni kijana mtulivu ambaye anaelewa nini anafanya. Hapendi competition ila kuna watu wanataka kufanya competition naye na kutaka kutengeneza jambo ambalo halina maana,” amesema Shilole.

“Ni kweli hakuna mtu aliyemjua Bill Nas kabla hajawa kwa TID lakini mimi naamini anamheshimu sana TID.”

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM