Thursday, 18 August 2016

SHEHE MKUU DAR AMUITA WEMA SEPETU KUHUSU ISHU YA MTOTO
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum amemuita Miss Tanzania 2006 na nyota wa filamu za Bongo, Wema Sepetu kufika ofisini kwake kwa ajili ya dua ili aweze kupata mtoto, Amani lilizungumza naye. Shehe Salum aliyasema hayo wiki iliyopita baada ya kupigiwa simu na paparazi wetu na kuulizwa kuhusu kilio cha Wema kila siku ishu ikiwa kukosa mtoto kwa umri wake wa miaka 28. Amani: Shehe, kwanza pole na kazi.


Mimi nilikuwa nataka kujua, wewe kama kiongozi mkuu wa dini ya Kiislam Mkoa wa Dar es Salaam, unasemaje kuhusu kilio cha msanii Wema Sepetu, kuhusu kukosa mtoto? Shehe: Hilo suala nadhani ni vizuri Wema mwenyewe akaja ofisini kwangu nikamuombea yeye mwenyewe baada ya kuzungumza naye. Lakini haiwezekani nifanye hivyo akiwa mbali.”
KUHUSU WEMA MWENYEWE Juzi, Amani lilimsaka Wema ili kumsikia anasemaje kuhusu wito wa shehe mkuu wa mkoa, lakini hakuwa hewani na hata alipotumiwa ujumbe kwa Mtandao wa WhatsApp hakujibu.
ALIANZA MCHUNGAJI
Hivi karibuni, Mchungaji Daudi Mashimo wa Huduma ya Injili ya Maumivu na Uponyaji iliyopo MbeziMsakuzi jijini Dar alikesha kwa maombi na kufunga akimuombea staa huyo apate ujauzito baada ya kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa, anakosa amani kwa kutopata mtoto huku baadhi ya mastaa wenzake wakimkejeli kwa vijembe. Hata hivyo, miezi ya karibuni, Wema aliwahi kudai ana ujauzito jambo ambalo liliwapa faraja mashabiki wake wakiamini kuwa, kilio chake kimefika tamati. Lakini miezi michache mbele, ikadaiwa mimba hiyo imetoka hali iliyozua maswali, wengi wakisema ilikuwa puto, kwa maana kwamba, WEMA HAKUWA NA MIMBA!!

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM