Friday, 26 August 2016

SEPTEMBA MOSI !! NI KAMA UBABE VILE KATI YA CHADEMA NA JESHI LA POLISI KUTUNISHIANA MISURI

Jeshi la polisi nchini limewataka wananchi kuwa watulivu na kuendelea na kazi zao bila hofu watakapoona vikosi vya jeshi vikifanya mazoezi mtaani kwa kuwa hayana lengo la kumdhuru mtu yeyote anayefuata sheria za nchi.

"Ili tuishi kwa amani ni lazima tutii sheria na kama hutaki kutii sheria tutashughulika naye, Kama kuna mtu anataka kuvunja amani katika mkoa wetu ajue kabisa hatoweza na niseme tu kwamba kama wanataka kujenga ukuta wajenge ukuta mwingine maana huu umeshadondoka".–Kamanda Sirro.
 
Aliongeza kwa kusema kuwa na wapo watu wanasema kwanini tunafanya mazoezi, nikwamba Jeshi la Polisi ni kawaida kufanya hivyo na muhimu watu wajue hiyo September 1 hakutakuwa na maandamano ya aina yoyote kwahiyo watu wasiwe na hofu bali wachape kazi.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM