Thursday, August 25, 2016

Romy afunguka Diamond kutokufika kwenye birthday yake

BAADA ya hivi karibuni ndugu wa Mwanamuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, kufanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuhudhuriwa na mastaa kibao isipokuwa msanii huyo na kudaiwa kuwa wana bifu, Romy Jones ‘DJ RJ’ ameibuka na kueleza kilichotokea.

Tetesi zilizagaa kwamba Diamond na Romy wana bifu ndiyo maana hakuonekana kwenye sherehe hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Next Door jijini Dar huku mastaa kama AY, Wema Sepetu na wengine wengi wakihudhuria ambapo Romy ameibuka na kueleza kuwa Diamond alikuwa na projekti muhimu studio ndiyo maana hakuonekana.

“Diamond ni ndugu yangu hatuwezi kugombana na mama zetu bado wako hai, wangekuwa hawapo labda hapo tungeweza kugombana. Sababu ya yeye kutohudhuria kwenye sherehe yangu ni kwamba alikuwa na projekti muhimu sana studio siku hiyo na ilipofika saa kumi usiku akataka aje nikamwambia asije ndiyo tunamalizia
.
Kifupi hatuna bifu kama watu wanavyosema, tuko vizuri kabisa,” alisema Romy.
BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

Total Pageviews

BONYEZA HAPO CHINI

TAZAMA FRANCIS CHEKA TV

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.