Sunday, August 28, 2016

Roma amtetea Professor Jay kwa wanaopinga kuhusu Hip Hop-Singeli

Muziki wa Singeli unaonekana kuwaumizwa kichwa wasanii wengi wa Hip Hop hasa baada ya Professor Jay kuachia wimbo wake mpya ‘Kazi Kazi’ aliomshirikisha Sholo Mwamba na kuamua kuuita style hiyo jina la Hip Hop Singeli.
Roma-1
Akiongea na kipindi cha E News cha East Africa TV, Roma Mkatoliki amemtetea Jay kwa kusema kuwa muziki wote umeshafanya inatakiwa msanii aje na idea yake mpya ya kuwateka mashabiki na kwamba kitu alichokitambulisha rapper huyo ni kipya siyo lazima kila mtu akikubali.
“Hata ukichukua akapela ya Jay ukaivalishie kwenye beat la ‘Zali La mentali’ itakuwa ni vile vile si rap?,” amehoji Roma.
“Kwahiyo hiyo ni combination kati ya Singeli na Hip Hop ambayo ni Hp Hop Singeli kama ambavyo yeye alivyoona kuita hivyo. Nafikiri ni kutambulisha kitu fulani, ukumbuke muziki kila mtu kashafanya kwahiyo inabidi uje na idea tofauti ambayo itateka attention ya mtu,” ameongeza.
“Kwahiyo unapotambulisha kitu kipya siyo kila mtu atakikubali.”
Mpaka sasa wimbo huo una takribani wiki nne tangu umetoka na umeshafanikiwa kutazamwa zaidi ya mara laki nne kwenye mtandao wa YouTube.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

Total Pageviews

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG PENDWA ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.