Thursday, 18 August 2016

Polisi Dar wametangaza kumtafuta Masanja Mkandamizaji

August 17 2016 Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam imewahoji wasanii wanne wa kundi la sanaa ya uigizaji Orijino komedi akiwemo meneja wao Seki kwa tuhuma za kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja.
Millardayo.com imempata kwenye exclusive interview kaimu kamishna wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam Hezron Gyimbi ambaye amesema hadi sasa bado wanamtafuta Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja.
Wamekamatwa jana saa 10 jioni ambapo wamehojiwa na wamekaguliwa sehemu wanazokaa kuona kama wana vitu zaidi ya uniform‘-Hezron Gyimbi 
Tunakamilisha hatua za kiupelelezi, makosa yanadhaminika wakipata watu wanaweza wakawadhamini sababu dhamana ni haki ya mtu‘-Hezron Gyimbi 
Jalada kesi ya wasanii orijinal komedi linaandaliwa litapelekwa kwa DPP, ndio mwenye dhamana ya kupeleka mahakamani‘-Hezron Gyimbi
Bado tunamtafuta Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ kwa sababu yule atakuwa shahidi muhimu sana kwetu;-Hezron Gyimbi

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM