Monday, 29 August 2016

Ole Sendeka: Lowassa ni mtu muungwana


Msemaji wa chama cha mapinduzi CCM, Christopher Ole Sendeka amesema Edward Lowassa ni muungwana kwa kusalimiana na Rais Dkt John Magufuli bila kinyongo.
maxresdefault Msemaji mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Christopher Ole Sendeka
“Namfahamu Lowassa ni muungwana hawezi kuacha kusalimiana kwa kupeana mikono na Rais, wamekutana viongozi, rais na waziri mkuu mstaafu hawawezi kuacha kusalimiana”, alisema Sendeka.
lowassa
Lowassa ni mjumbe kamati kuu ya CHADEMA aliyechuana na Dk Magufuli katika uchaguzi mkuu 2015 mwaka jana, na juzi walikutana kwa mara ya kwanza na mpinzani wake huyo.
Viongozi hao walikutana katika Jubilee ya miaka 50 ya rais mstaafu Benjamin Mkapa katika kanisa la Mtakatifu Petro, lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
CHANZO: MWANANCHI
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM