Tuesday, 16 August 2016

Mzee Yusuf kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji baada ya kuachana na muziki


Baada ya hivi karibuni Mzee Yusuf kutangaza kuachana na kufanya muziki, ameweka wazi kuwa kilimo na ufugaji ndiyo kimbilio lake. DIAMONDNAMZEEYUSUF1
Muimbaji huyo mahiri wa taarab alitangaza azma hiyo Ijumaa iliyopita kwenye msikiti wa Taqwah jijini Dar es Salaam huku akidai kuwa kuanzia sasa atakuwa akimtumikia Mungu zaidi.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Mzee Yusuf amesema baada ya kuachana na kufanya muziki anaenda kujikita na kilimo pamoja na ufugaji.
“Nimeacha kwa ridhaa yangu mwenyewe,” alisema Mzee Yusuf. “Ni mimi mwenyewe nilikaa nikaamua niachane na muziki nitafute vitu vya halali nifanye ili niwe nafanya ibada vizuri,”
“Kwa sababu nilikuwa naswali lakini nahofu, kwa sababu muziki ni haramu. Kwa hiyo sasa hivi nitafanya biashara nyingine, nitakuwa nafuga, nimeanza pia kulima, kwa ufupi nitakuwa mkulima,” aliongeza.
Wimbo wa mwisho alioutoa Mzee Yusuf ulikuwa Hewallah aliomshirikisha Vanessa Mdee.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM