Wednesday, 17 August 2016

Mzee Yussuf Ataendelea Kusikika Japo Anasema Amestaafu Muziki - Khadija Yusuf

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mzee Yussuf kutangaza kuacha rasmi kazi ya muziki na kumrudia Mungu, mdogo wa mzee Yussuf, Khadja Yussuf ambaye ni muimbaji katika bendi ya Jahazi Modern Taraab amefunguka na kusema Mzee Yusuph lazima atasikika.

Khadja Yussuf
Amesema kuwa licha ya kaka yake huyo kuacha muziki lakini 'band' hiyo itaendelea kufanya kazi ya muziki na wataendelea kutoa kazi ambazo Mzee Yussuf alishiriki.

Akiongea kwenye kipindi cha eNewz ya EATV Khadja alisema kuwa ni kweli mzee amemrudia Mungu lakini jambo hilo haliwazuii wao kuendelea na kazi ya muziki na kudai Mzee Yussuf atake asitake lazima katika baadhi ya kazi ambazo tayari alishafanya kwenye bendi hiyo ataonekana tu kwani hawawezi kufanya marekebisho na kumuondoa katika kazi hizo ambazo zinatarajiwa kutoka siku za karibuni.

"Hata kama Mzee amemrudia Mungu muache huko huko na Mungu wake, lakini sisi tutaendelea kufanya kazi na kutoa kazi nzuri zaidi hata ya hizo, kwani waimbaji wapo wengi siyo mzee tu, nachoweza kusema ni kwamba kuna kazi ambazo tulishafanya na Mzee Yussuf nyingine amepiga kinanda kwenye wimbo wa mkewe, na nyingine ameonekana au ameimba, hizo kazi zitaendelea kutoka, tunachoweza kufanya tunaweza kuondoa picha yake kwenye band lakini kazi ambazo ameshiriki lazima ataonekana tu zitakapotoka hilo hawezi kulikwepa" alisema Khadja Yussuf

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM