Saturday, August 20, 2016

Mtoto aliyezaliwa ndani ya ndege ikisafiri apewa Makubwa

MTOTO aliyezaliwa ndani ya ndege iliyokuwa ikisafiri angani ametunukiwa zawadi ya kilomita 1.6 milioni ambazo atasafiri bila kulipa nauli katika ndege za shirika la Cebu Pacific atakapokuwa mkubwa.
Mtoto huyo, Haven, alizaliwa wakati ndege ya shirika la Cebu Pacific la Ufilipino, ilikuwa ikisafiri kutoka Dubai kuelekea Manila.
 
 
Kulingana na madaktari, mama ya Haven alijifungua mnamo Agosti 14, wiki tano mapema kabla ya muda wake kuwadia.
Wauguzi wawili ambao walikuwa wameabiri ndege hiyo walimsaidia mwanamke huyo kujifungua. Rubani wa ndege hiyo alitua ndege hiyo kwa dharura katika uwanja wa Hyderabad, India ambapo mwanamke huyo alipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Kulingana na shirika la CNN, mkurugenzi wa Cebu Pacific, Lance Gokongwei, alimtuza mtoto huyo maili 1,000,000 ambapo atasafiri bila kulipia tiketi kama zawadi ya kuzaliwa.
"Tunafurahi sana kwani mtoto na mama yake wanaendelea vyema kiafya,” akasema mkrugenzi huyo.
Zawadi hiyo inamaanisha kuwa mtoto huyo anaweza kwenda na kurudi nchini Amerika kutoka Kenya mara 32.

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

Search This Blog

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Total Pageviews

WATCH LEWIS MBONDE TV ONLINE

BOOK NOW MAMA G CATERING WAPISHI BORA WA SHEREHE BUSINESS NO:0754 887265 0652 887267 0673 538583

Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.