Wednesday, August 24, 2016

Mr Blue: Barakah na Naj walitaka kunivunjia ndoa yangu


Mr Blue amekiri kuwa skendo yake kuwa amekuwa akiwasiliana na ex wake, Naj ambaye kwa sasa ana uhusiano na Barakah Da Prince ilitaka kuivunja ndoa yake.
love
Akiongea na Clouds FM, rapper huyo wa ‘Mboga Saba’ amedai kuwa mke wake, Wahyda sasa amekuwa na wivu wa kufa mtu tangu kuzuke skendo hiyo.
“Sasa hivi naona kama wivu umezidi baada ya hii skendo ya hawa jamaa kuitengenezea kiki kwasababu wanataka kutoa nyimbo yao, skendo kwamba mimi nilimpigia yule mwanamke mwingine nani anaitwa, Najma yule. Wametengeneza kweli kabisa, mimi nimezipata za kunyapianyapia kwamba wametengeneza ili kukikisha nyimbo zao,” amesema Blue.

“Lakini wamenikosea sana kwasababu wanataka kugombanisha ndoa yangu, mimi nina mke ujue, siwezi kumpigia mtu ambaye nimemwacha, ni kosa kubwa sana, halafu mke wangu yule ni mwanamke ambaye walikuwa watatu kupigania nani awe na mimi, yaani bora hata ningempigia mtu mwingine,” amesisitiza.
11265242_1017376255008074_128804752_n
“Ilifika karibu kama siku mbili tuna ugomvi mimi na mke wangu, ni kitu kikubwa sana, nimekasirika sana, nimechukia sana na nawaambia mashabiki wangu, alichokifanya Barakah na watu wake, kama sio yeye simlaumu, kama watu wake nilikuwa naomba waoneshe proof kwenye mitandao waoneshe namba yangu niliyompigia, waioneshe kwamba ni hiyo kweli sio unaongeaongea tu.”
Skendo hiyo ilianza baada ya Barakah kudaiwa kushika simu ya mpenzi wake Naj, alipiga mtu ambaye namba yake ‘iliseviwa’ Zai na baada ya Barakah kupokea alikuta sio mwanamke bali ni mwanaume ambaye alidaiwa kuwa ni Mr Blue.

BONYEZA HAPO CHINI KUITAZAMA FRANCIS CHEKA TV
Share:

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA KUHUSU HABARI HII

ANGALIZO:TUNAOMBA UTUMIE LUGHA NZURI MAONI YENYE LUGHA CHAFU HAYATAKUBALIKA

BONYEZA HAPO CHINI

Total Pageviews

WATCH FRANCIS CHEKA TV

OWNER:LEWIS MBONDE

Mawasiliano Yangu +255 658 194 194 Email:lewismbonde@gmail.com Kama una habari tafadhali tutumie kupitia email yetu Morogoro,Tanzania

HABARI MPYA


Recent Posts Widget

Translate

Blog Archive

FIND US ON FACEBOOK

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

BLOG ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.