Friday, 26 August 2016

MORO KIDS U17 WAIBUKA MABINGWA WA AIRTEL RISINGI STARS MOROGORO 2016

Wachezaji wa timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (U17) ya Moro Kids Academy wakifurahi huku wakiwa na kombe la ubingwa michuano ya Airtel Risng Stars baada ya kuifunga Anglikana Academy katika mchezo wa fainali bao 1-0 uwanja wa jamhuri Morogoro. Picha na Juma Mtanda,
 
Juma Mtanda, jphtjuma@gmail.com
Timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (U17) ya Moro Kids imetwaa ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars baada ya kuikung’uta Anglikana Academy bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.ali lililojaa wavuni kufuatia pasi ya Michael Jeremiah dakika ya 59 ya mchezo huo.

Mashindano hayo yalishirikisha timu sita za Mwere Kids, Kizuka Sekondari Ngerengere, Jabal-Hira Sekondari, Tekfot, Moro Kids na Anglikana Academy yaliyoanza kutimua vumbi Augost 17 mwaka huu kwa lengo la kusaka vipaji vya kuunda timu ya mkoa wa Morogoro ya Airtel Rising Stars itayoshiriki mashindano ya taifa.

Naye Katibu Msaidizi wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) Jimmy Lengwe alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa na tija kubwa Tanzania kiujumla kutokana na kuendeleza vipaji vya vijana na kuiomba kampuni ya simu za kiganjani ya Airtel kuongeza idadi ya timu katika mikoa.

Lengwe alisema kuwa Morogoro pekee ina vituo vingi vya katika wilaya zinazounda mkoa huo hivyo endapo Airtel itaongeza wigo wa kuongeza timu zinazorishiki mashindano hayo itakuwa imefungua njia ya kuibua vipaji vingi vya soka kwa vijana ambao bado hawajaonekana.

“Michuano ya Airtel Rising Stars ni michuano inayoendeleza kuibua vipaji vya soka kwa vijana hapa nchini lakini ningeomba michuano ijayo ngazi ya mikoa ziongezwe idadi za timu zinazoshiriki ili kuendelea uibuaji wa vijana hasa waliopo wilayani”alisema Lengwe.

Lengwe alisema kuwa baada ya kumalizika kwa michuano hiyo tayari majina 19 yameteuliwa ili kupata majina 16 yatayounda timu ya mkoa wa Morogoro ya Airtel Rising Stars.

Majina ya wachezaji walioteuliwa kuingia katika majina ya mchujo ni pamoja na Silveter Oscar kutoka Kizuka, Abdi Rashio , Jabal-Hira, Salum Likwala, Maimil Hamis, Filipe Abel, Idrisi Athman na Kipa kutoka Tekfot wakati kipa, Alex Gidion akitokea Anglikanai.

Wengine ni, Teps Evans na Theomis Dickson wakitokea Mwere Kids Academy huku Moro Kids wakichaguliwa wachezaji, Michael Jaremiah, Jamal Juma, Rajabu Mustafa Azizi Rashid, Abdu Hassan, Ibrahim Yohana, Bonifase Joseph na Aman Rajabu kipa.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM