Wednesday, 17 August 2016

Manji atuma ujumbe kwa mashabiki wa Yanga

Yusuf-Manji-002
Habari ya Yusuf Manji kujiuzulu kwenye nafasi yake ya uenyekiti ndani ya klabu ya Yanga ndio imekuwa stori kubwa ikiwa ni siku chache tangu atangaze kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka kumi.
Manji alifikia maamuzi hayo baada ya kuona kuwa anashutumiwa vibaya na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali na viongozi wengine wa Yanga na kumpelekea kukaa pembeni ili kulinda heshima yake.
Kitendo hicho kimepokelewa kwa huzuni na jaziba na mashabiki pamoja na wanachama wa timu hiyo Jumanne hii ya Agosti, 17 walikutana katika makao makuu ya klabu yao na kukubaliana kumsimamisha uanachama Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali ambaye alidaiwa ndiyo aliyechochea Manji kuchukua uamuzi huo baada ya kuzungumza katika vyombo vya habari kuwa Manji amekurupuka.
Baada ya hayo yote, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa Yanga aliyefungiwa na TFF, Jerry Muro ametoa taarifa kutoka kwa Manji ambayo amemwagiza aifikishe kwa mashabiki wa klabu hiyo inayozungumzia hatma ya mahusiano yake na Yanga.
“Jerry waambie wana Yanga pamoja na vurugu zote hizi nitaendelea kuwa upande wao na kamwe sitawaacha nguvu yangu iko kwa wanachama,wapenzi na mashabiki”-Bw Yusuf manji,” ujumbe wa Manji kwa mashabiki wa Yanga.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM