Saturday, 20 August 2016

Malkia wa Taarabu Shakila Saidi afariki dunia jioni ya leo

Habari za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya leo muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam.
 
 Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vilivyo karibu na marehemu, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali akakata roho.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM