Thursday, 25 August 2016

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi Italia yaongezeka hadi watu 247

Idadi ya watu waliofariki kwenye tetemeko la ardhi lililotokea nchini Italia Jumatano hii imeongezeka na kufikia watu 247.
378D44F900000578-0-image-a-6_1472081701301
Tetemeko hilo linalokadiriwa kuwa na nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Ritcher limesababisha madhara makubwa kwenye miji ya Umbria, Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto kwa watu kufukiwa kwenye vifusi.
Wakati maafisa wa uokoaji wakiendelea na juhudi za kuwaokoa watu walionusurika kwenye tukio hilo walitatizwa na mitetemeko mingine iliyotokea ghafla na kutikisa majumba yaliyosalia yakiwa bado wima.
Maeneo yaliyokumbwa zaidi na uharibifu huo ni Accumoli na Pescara del Tronto huku tetemeko hilo likitajwa kuanzia kwenye Norcia, kilomita 170 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Roma.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM