Saturday, 1 July 2017

FAHAMU MAANA YA BRAND NA NAMNA UNAVYOWEZA KUJI-BRAND


http://storage.googleapis.com/thinklegacy/images/gdn-brand-solutions_products_sm.jpg
Na Lewis Mbonde +255 658 194194
Kama unataka kuanzisha biashara, au umekwisha anzisha, basi hii mada inakuhusu. Na hata unataka kuajiriwa au unatafuta kazi bora zaidi uliyonayo, ni jambo la msingi kujua namna ya kuwa na Brand inayouzika.

Maana ya Brand
Branding ni namna ya kutengeneza HISIA chanya mbele za hadhira. Ni namna unavyotaka wafikirie na waitambue bidhaa husika au asasi.
Mfano ukisikia Dr Cheni unapata picha kuwa ni msanii mkongwe katika kiwanda cha filamu ambaye anaelimisha na kuburudisha jamii. Ndio kusudio lake kuu.

Kuna mengi ya kufanya ili kujenga hisia hizo- jinsi unavyowasiliana na hadhira , huduma kwa wateja, aina ya bidhaa zako, uwajibikaji wako kiutendaji n.k

Hii sio maana ya Brand
Brand sio rangi , sio logo(nembo), sio jina la bidhaa. , bali ni nini vitu kama hivyo vina leta hisia na vinasadia kufanikisha lengo la uwepo wa bidhaa/asasi au mtu husika.

Kwanini unahitaji kuwa na Brand
Kama tulivyoona katika maana ya Brand, lengo kuu la Brand ni kufanikisha kukubaliwa mbele ya wale unaowalenga, hivyo basi unahitaji Brand ili kujiwezesha kupata kazi bora unayoihitaji kwani kwa picha nzuri utakayoijenga kwa jamii , unaweza kupata watu watakaotaka kufanya nawe kazi.
Pia Brand inakusaidia pale unapotaka kuanzisha biashara , au kama tayari unayo biashara basi inakurahisishia kuuza bidhaa zako nyingine mpya.
Brand inakufanya ujenge mtandao na watu wa muhimu katika fani yako, ajira na biashara.

Je unatengeneza Brand yako ?
Kwanza kabisa inabidi ujijue unapenda kufanya nini na nini utakachotoa kwa jamii kama bidhaa. Mfano kama lengo lako ni kutoa huduma za michezo mfano mpira wa miguu, basi utajikita katika kujifunza kwa undani kuhusu mambo ya mpira wa miguu, kushiriki katika michezo na kushare habari za kina kuhusu mpira wa miguu.

Hata hivyo haitoshi tuu kuonekana upo fiti katika hicho bidhaa yako , bali pia uwafanye watu wengine wapende kuwa karibu nawe. Hapa ndipo kazi ya ziada inahitaji katika namna yako ya kufanya mawasiliano.
Kumbuka mawasiliano ni zaidi ya unachozungumza, hata namna ya mavazi yako, lugha yako, umakini wako, tafakari zako, jinsi ulivyo wa msaada, mtandao wako n.k vyote vitakusaidia kujitengeneza kama BRAND.

Jitokeze ufahamike
Kujifunza na kuwa na kitu cha maana cha kutoa kwa jamii hakutoshi kama haujafahamika na kuanza kujenga Brand. Tafuta nafasi ya kuzungumza na makundi ya watu unaowalenga.
Tumia mitandao ya kijamii kwa faida ili kuifanya jamii ikutambue kwa namna unavyolenga kuja kutoa bidhaa yako.

Hitimisho
Fikiria na amua leo, je wewe unataka kutambulika kama mtu wa namna gani? Anza kujijenga kama BRAND !
Kumbuka tunatengeneza BRANDS ili kunufaika hususani kifedha na kimaendeleo. Haijalishi muda gani utachukua kabla ya kuweka BRAND imara, ila kumbuka INALIPA kufanya hivyo.
Waweza jibrand kama MTU MAKINI, MWAMINIFU, MCHAPAKAZI halafu uone matokeo yake. Ila inahitaji kazi na mikakati kufikia huko.

Mawasiliano +255 658 194 194

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers

FOLLOW ME ON INSTAGRAM