Latest Posts


Saturday, December 10, 2016

Tuesday, December 6, 2016

BREAKING NEWZZ:Hatimaye Diamond na Zari Wamepata Mtoto wa Kiume Leo Tarehe 6 Dec 2016

Ni good news nyingine kwa msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye leo December 6 2016 mpenzi wake Zarina Hassan amefanikiwa kujifungua mtoto wake wa pili, Zari na Diamond wamepata mtoto wao wa pili baada ya kupata mtoto wao wa kwanza Tiffah August 2015.
HONGERENI SANA ZARI NA DIAMOND!

Mzee wa Miaka 75 Ameweka Bango Lenye Sifa za Mke Anayemtaka, Katikati ya Mtaa Anaoishi


Mzee wa miaka 75 nchini Tanzania ameweka bango lenye sifa za mke anayemtaka, katikati ya mtaa anaoishi.
Athuman Bakari Mchambua mkazi wa Dar es Salaam amechukua hatua hiyo baada ya kifo cha mke wake.
Amesema hawezi kutumia njia nyingine yoyote isipokua udahili ama mahojiano kumpata mke. - BBC

OP 5 ya Wasanii wa Bongo Waliomake Mkwanja Mrefu Kwa Huu Mwaka 2016

1.Diamond
Huu jamaa katengenza hela nyingi sana mwaka kuanzia kwny endorsement zake, show, kuuza mziki kwny digital platform plus label yake inayomwingzia mkwnja day after day

2.A.Y
Japo jamaa hategemei sana kwenye mziki kwa asa ivi ila kutokana na miladi yake kwa mfano ana kipindi eatv ambacho kwa mtazamo tu wa kawaida kinamwingizia mpunga wa kutosha kabisa

3.Weusi
Hawa jamaa nao kwa huu mwaka ulikuwa poa sana kwako maana wametoa ngoma Kali sana ambazo zimewapatia show za kutosha na zenye mkwanja mwingi

4.Navy kenzo
Hawa jamaa ni kati ya makundi yanoyofanya vizuri sana kwny huu mziki wa bongo flava na wamewaza kupata endorsement airtel ambayo nahisi iliwatengenezea mkwanja mwing sana plus wana studio yao the industry ambayo nayo inaingiza mpunga wa kutosha

5.Lady Jay dee
Binti machozi ukipenda mwite komando au anaconda, tokea arudi na ngoma yake ya ndi ndi ndi baada ya kukaa kimya takriban mwaka mmoja imemuweka pazuri kufanya show za kutosha tena zake yeye mwenyewe plus show kali kabisa aliyoifanya pale mlimani city ambapo kiingilio cha chini ilikuwa 50,000Tsh.

Huwo ndo mtazamo wangu
By Isho_boy

DAVIDO ASEMA HAYA KUHUSU POST HII YA DIAMOND PLATNUMZ

Kwa Davido, Tanzania itaendelea kukaa katika nafasi muhimu sana moyoni mwake.

Katika wakati ambao wengi tunadhani ameisahau, hitmaker huyo wa How Long, ameibuka na kuthibitisha kuwa bado ana mapenzi tele na ya milele kwa nchi ya Magufuli.
davidoofficial-20161017-0001
Davido
Ameufungua moyo wake kwenye post ya Diamond katika mtandao wa Instagram ya show yake ya mjini Harare nchini Zimbabwe – Watora Mari iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Kwenye post hiyo ya show hiyo iliyofana na kushuhudia akiujaza ukumbi mkubwa wa HICC akiwa na mwenyeji wake Jah Prayzah, Diamond aliandika:
This Song Called #NumberOneRemix it has more than 18.5 Million Views on Youtube….. Go watch it and enjoy the Mix of Bongo flavour and Naija.”

Kama ambavyo Jah Prayzah anamshukuru Diamond kwa kumtambulisha kwenye ramani ya muziki wa Afrika, Diamond atamshumkuru milele Davido kwa kumpa shavu kwenye remix ya Number One iliyompa staa huyo wa Tanzania umaarufu mkubwa
PicsArt_12-05-08.35.18

Jiji la Dar es Salaam Lashika Nafasi Ya 6 Barani Afrika Kwa Maambukizi Ya Ukimwi

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mbali na jitihada za makusudi za Serikali na wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI nchini bado hali siyo ya kuridhisha ambapo Jiji la Dar es Salaam linashika nafasi ya Sita barani Afrika kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Dar es Salaam ambalo ni Jiji kubwa kuliko yote Tanzania linakadiriwa kuwa na watu 210,000 wanaoishi na virusi vya UKIMWI ambapo kati yao asilimia 58 ni wanawake, na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wa jiji hilo inakadiriwa kuwa Milioni 5.
 Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani kutoka Shirika la Mpango wa UKIMWI la Umoja wa Mataifa - Tanzania (UNAIDS) kwa mwaka 2015, Jiji la Dar es Salaam limekuwa kati ya majiji Barani Afrika yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya UKIMWI.

Afisa wa UNAIDS Tanzania, Fredrick Macha anasema asilimia 16 ya maambukizi yote mapya Tanzania Bara yanatokea katika jiji la Dar es Salaam ambapo kwa wanawake wenye umri mdogo wa miaka 15-24 kiwango cha maambukizi kimefikia asilimia 7%,sababu kubwa ikiwa ni kujiingiza katika ngono wakiwa na umri mdogo pamoja na biashara ya ukahaba.

Anafafanua kuwa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto Jijini Dar es Salaam ni asilimia sita (6%) licha ya jitihada kubwa za Serikali na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI,kuelimisha na kuhamasisha wajawazito kupima na kufuata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga na VVU.
“Takwimu za Wizara ya afya za mwaka (2011-2012), mtu mmoja kati ya watu watano jijini Dar es Salaamana mahusiano ya kimapenzi na zaidi ya mtu mmoja,na mara nyingi wanafanya ngono zisizo salama hivyo hicho ni kiashiria kikubwa cha ongezeko la maambukizi hasa kwa wana ndoa”alisema Macha.
 Aidha amevitaja baadhi ya vichocheo na viashiria vinavyochangia uwepo wa ongezeko kubwa la maambukizi katika jiji hilo kuwa ni ukuaji wa kasi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara unaosababisha muingiliano wa watu kutoka Mikoa mbali mbali nchini pamoja na mataifa mengine.
Dar es Salaam kama yalivyo majiji mengine duniani yenye muingiliano wa tamaduni na desturi mbalimbali limeathirika pia na makundi yanayoelezwa kuchochea maambukizi mapya ya UKIMWI kama vile wafanya biashara ya ngono, wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na watumiaji wa madawa ya kulevya na kwa kujidunga.
                                                                                     
“Kwa mujibu wa takwimu hizo, kati ya wanawake 4 wanaojihusisha na biashara ya ngono, mmoja ni mwaathirika na virusi vya UKIMWI (sawa na asilimia 26).Vile vile kati ya watu watano wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, mtu mmoja ameathirika, sawa na asilimia 22.3) na kati ya watu sita wanaotumia madawa ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindano, mmoja ni mwathirika wa virusi vya UKIMWI (sawa na asilimia 15.5),”alisema Macha.
 Aidha Macha alisema pamoja na changamoto mbalimbali, Jiji la Dar es Salaam limependekezwa kuwa moja ya majiji machache ya mfano ulimwenguni katika mkakati wa dunia wa kuimarisha udhibiti wa UKIMWI kwenye majiji (UNAIDS Fast Track Cities Initiative).
 Mkakati huo ni kuyafanya majiji makubwa Afrika kuwajibika zaidi katika kuongeza ufanisi kwenye mapambano dhidi ya UKIMWI katika maeneo ya mijini kwani kasi ya maambukizi na wingi wa maambukizi yapo mijini.
 Pamoja na majiji kuwa na rasilimali nyingi, mifumo ya utoaji huduma za afya bado inaandamwa na changamoto mbalimbali, hususani katika kuandaa na kutekeleza mipango mizuri yenye kuhakikisha ushirikishwaji wa watu wote hasa makundi maalumu katika jamii, ambayo kiwango cha maambukizi ni kikubwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama anasema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake  nchini wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume,jambo ambalo linahitaji jitihada zaidi kujikinga.

“Kwa mujibu wa Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.

Waziri Mhagama anasema kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa  kuwa  jumla ya watanzania 1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati ya 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.

Aliongeza kuwa UKIMWI bado ni janga kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa  maambukizi mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000 kwa mwaka hali ambayo  inaashiria kupoteza  nguvu kazi kubwa katika nchi yetu hivyo Tanzania itendelea kushirikiana na nchi nyingine Duniani,pamoja na mashirika ya kupambana na UKIMWI kuhakikisha janga hilo linatokomezwa  ifikapo mwaka 2030.

Alisema Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza kupima afya zao kwa hiari ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika kuwa na VVU,bila kusubiri hadi kinga zao zipungue.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko alisema kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa Watanzania 2,100,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya sasa lakini  pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.

”Ingawa maambukizi ya VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382, Watanzania hatutakiwi kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za pamoja kuhakikisha janga hili linafikia mwisho,”alisema Dr. Maboko.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu alisema wataalam wa afya wametuambia UKIMWI unapungua nchini Tanzania, suala hilo linatokana na misaada mbalimbali tunayoipata kutoka nchi wahisani  kwahiyo ili kutokomeza kabisa suala la upungufu wa dawa na misaada kwa waathirika wa ugonjwa huo Watanzania wanahitaji kujichangia wenyewe na sio kutegemea fedha za wahisani peke yake.

Alifafanua kuwa ili kuwezesha suala hilo,Sheria Na. 5 ya mwaka 2015 imeitaka Wizara yenye dhamana kuwa na Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI pamoja na Bodi yake hivyo, kuanzishwa kwa Mfuko huo kutaleta chachu kwa Watanzania kuungana kuzuia maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI (VVU) pamoja na kuwahudumia wananchi wanaoishi na virusi hivyo.
 “Kwa kawaida fedha zinazotoka kwa wahisani huwa zina mwisho wake hivyo Tanzania tunazindua Bodi rasmi itakayosimamia Mfuko huo ili na sisi tuongeze nguvu pale wahisani watakapoishia,”alisema Mama Samia.
 Naye muathirika wa UKIMWI, (jina limehifadhiwa) ameishkuru Serikali kwa kuwasaidia kwa hali na mali watu wenye ugonjwa huo kwani sio wote wenye ugonjwa huo wameupata kwa kujitakia.
 “Kitendo hiki kinatufanya tusijione wanyonge wala kukata tamaa kwani Serikali yetu haitutengi inatupa ushirikiano sawa na watu wengine wasio na maambukizi ya ugonjwa huu,”alisema muathirika huyo.
 Tarehe 1 Disemba kila mwaka ni siku maalumu ambayo tunaadhimisha Siku ya UKIMWI duniani, siku ambayo kwa pamoja tunaungana na watu wote wanaokadiriwa kufikia milioni 78 ambao tayari wameshapata mambukizi na watu milioni 35 ambao tayari wamefariki ulimwenguni kote kutokana na athari zitokanazo na maambukizi ya UKIMWI.

Ajali Mbaya ya Lori na Hiace Yaua Watu 9 na Kujeruhi 18 huko Ifunda Iringa

Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugonga gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace. 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace hiyo iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara. 
“Lori limeharibika kabisa na Hiace pia imeharibika kabisa,” alisema Kamanda Masenza. 
“Lori hilo liliposhindwa kufunga breki liliigonga Hiace ambalo lilikuwa na abiria na kwenda mbele na kisha kugonga watembea kwa miguu,,” 
Masenza alisema katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni, madereva wa magari hayo wote wamejeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi wengine. 
“Dereva mmoja yupo chumba cha upasuaji kwa kuwa mguu wake umevunjika na mwingine yupo wodini,” alisema 

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Alia na 'Utapeli' Vyeti vya Ndoa


Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mohamed Utali ametoa agizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Florent Kyombo kutomhamisha mwalimu yeyote kwa kigezo cha cheti cha ndoa. 
Alisema baadhi wanaghushi vyeti hivyo na vya maradhi ili wapate nafasi ya kufundisha kwenye shule zilizopo kando mwa barabara kuu na mijini hivyo kusababisha shule zilizopo mbali kukosa walimu. Utali alisema hayo jana alipofungua baraza la madiwani. 
Alisema shule zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya darasa la saba ni zilizopo mbali na barabara kuu na zenye upungufu wa walimu. 
Mkuu huyo wa wilaya ambaye kitaaluma ni mwalimu alisema anafahamu mbinu na ujanja wanaofanya baadhi ya walimu wanaotaka kufundisha shule za barabarani. 
“Mwalimu atakayekuja na kimemo cha kiongozi, ama cheti cha ndoa au ugonjwa na kuomba afundishe shule iliyopo kando mwa barabara kuu usikubali kumhamisha, tutumie madaktari tuwapime tujue hayo maradhi yao,” alisema Utali. 
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jonas Van Zeland alimtaka mkurugenzi kuwafuatilia walimu watoro na wanaoshindwa kukaa jirani na shule wanazofundisha kwa madai kuwa mazingira siyo rafiki. 
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kyomba alisema katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu, Wilaya ya Mvomero imeshika nafasi ya sita kimkoa na shule zilizofanya vibaya ni zenye uhaba wa walimu. 
Alisema atahakikisha anafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye shule hizo na kuwaomba wazazi, walezi na viongozi wengine wa kata na vijiji, pamoja na madiwani kumpa ushirikiano.

IRENE Uwoya Afunguka Haya Baada ya Gazeti Moja Kudai Anamchukia Wema Sepetu

Baada ya gazeti la Ijumaa kutoka na stori “Uwoya: Simpendi Wema” katika ukurasa wake wa mbele, muigizaji wa filamu Irene Uwoya amekanusha madai hayo kupitia ukurasa wake wa instagram.

Pia muigizaji huyo amedai yeye hana tatizo na Wema na sio mtu wa kuwekeana chuki na msanii mwenzake.

Kupitia instagram, Irene aliposti kipande cha gazeti hapo juu na kuandika

“Jamaniii sijawah sema simpend wema… Sina sababu ya kumchukia mim na mpenda kila Mtu na sinaga adui na wala sipend Kuwa na maadui na penda sana kuishi na watu vizuri… Hivo Ndivo nilivyo.”

Pia muigizaji huyo amedai wakati mwingine bifu huanzisha na waandishi wa habari pamoja na mashabiki.

Search This Blog

Total Pageviews

BLOGGER:LEWIS MBONDE


HOTLINE:+255658194194

Email:lewismbonde@gmail.com
Morogoro,Tanzania
Nakaribisha maoni yenu.Kama una habari pia
waweza kututumia kwenye email yetu hapo juu


Translate

FOLLOW ME ON INSTAGRAM

FIND US ON FACEBOOK

TUNATEMBELEWA DUNIANI KOTE

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Blog Archive

FLAG COUNTER

Flag Counter

BLOG PENDWA ZA MARAFIKI

Powered by Blogger.